PIKIPIKI hivi sasa imekuwa ni chombo cha kutegemewa katika usafiri wa abiria Tanzania. Hakuna utakapofika usikute stendi ya pikipiki.
Hali hii imesababishwa na wingi wa magari na jamu zinazoandamana nazo mijini, barabara mbovu sehemu kadhaa nchini na unafuu wa gharama kwa pikipiki kama chombo cha usafiri.
Pikipiki nyingi zinatoka China na ubora wake hauridhishi. IPO HAJA YA WATANZANIA WALIOKO NJE NA WENYE UWEZO kuja pamoja na kutafuta mtengenezaji pikipiki atakayekuja kuwekeza nchini.
Sasa ni ruksa yeye kuagiza viungo vyote vya pikipiki toka nje na akaziunganisha hapa hapa nchini na kuna mafundi wa kutosha kufanya kazi hiyo na kwa gharama nafuu. Kulingana na bei na ubora wa pikipiki atakazozalisha soko lote linaweza kuwa lake.
Facilitation ?
Contact:: ni.mailla@gmail.com
No comments:
Post a Comment